About us

New Music

View All

Pictures

Entertainment

View All

Video

Follow Us

Join the Club

 photo addspace.png

Ads

Contact Form

Name

Email *

Message *

Blogroll

Category 3

Category 6

Flickr Images

Category 4

Category 7

Label

Sports

Entertainment

Entertainment

Powered by Blogger.

Latest News

You are here: Home / G-Nako Azungumzia Sababu Za Kuwalipisha Wasanii Kufanya Collabo, Na Tofauti Ya Bei Zake

G-Nako Azungumzia Sababu Za Kuwalipisha Wasanii Kufanya Collabo, Na Tofauti Ya Bei Zake

| No comment
Mweusi G Nako hivi karibuni alitangaza kuanza kuwalipisha wasanii wanaotaka kumshirikisha kufanya chorus katika nyimbo zao. Kumbuka G-Nako anatajwa kuwa msanii anaefanya chorus nzuri zaidi za hip hop Tanzania na inadhihirika kwa kila wimbo anaopita.
fradohmusic.com imepiga story na G- Warawara kutaka kufahamu sababu zilizompelekea kuchukua uamuzi huo. “Yaani sasa hivi muziki umekuwa ni kazi vilevile ni biashara. Kwa hiyo biashara ni mimi mwenyewe, yaani mimi mwenyewe ni biashara. Kwa hiyo nikifanya kazi na wewe ni kama nimechukua biashara yangu nimeileta kwako. Kwa hiyo tunauza bidhaa. Tukijumlisha pamoja tunakuwa tunauza bidhaa. Kwa hiyo tunapotaka kuuza bidhaa lazima faida ipatikane sehemu zote mbili. Hilo ndilo lengo kubwa.” Akielezea mfumo wa bei aliojiwekea, G-Nako amesema bei yake haitofautiani sana kati ya msanii mkubwa na msanii mdogo, ni makubaliano ya kawaida tu anayofanya bila kujali. Amesisitiza kuwa kigezo kikubwa kwake ni wimbo mzuri na kuhakikisha inatoka kazi nzuri siku zote kabla ya kupanga malipo. “Pamoja na yote hayo lazima tutengeneze muziki mzuri. Kwa hiyo mimi kitu kikiwa kwenye feeling zangu mara nyingi huwa nakifanya nikiona kitu kinataka kuwa kizuri mara nyingi huwa nakifanya. Ni kama ambavyo kuwa nakuambia siku zote mnapokutana wasanii wawili wazuri lazima mtatengeneza kitu kizuri.”