Pages

Monday, June 23, 2014

Alicia Keys Awa Kisura Mpya Wa Manukato Mapya

Uzuri wa Alicia Keys plus jina kubwa alilopata kupitia kazi zake vimempa deal ya kuwa kisura kwenye manukato mapya ya kampuni maarufu duniani kwa manukato Givenchy.

 Sura ya muimbaji huyo wa “Girl on Fire” ataikuwa kichocheo cha mauzo ya perfume mpya ya kampuni hiyo iliyopewa jina la Dahlia Divin.
Hata hivyo bado hajajulikana ni kiasi gani cha pesa alicholipwa kuwa kisura wa pafyumu hiyo ambayo matangazo yake yataanza kuonekana kwenye majarida September mwaka huu.
Baadhi ya watu maarufu waliowahi kuwa visura wa pafyumu hiyo ni pamoja na Justin Timberlake, Liv Tyler, Uma Thurman, na Amanda Seyfried.

No comments:

Post a Comment